Saturday, June 2, 2012


MTUKUTU  HUTUKUKA, NAYE  MUI  HUWA  MWEMA

Kipi cha mno nduyangu, kiwashacho moyo wako?
Lipi lakuudhi langu, n’sielekeze kwako?
Yupi ni mwandani wangu, asohitajika kwako?
Simwone nyungunyungu, ana yake mipango.

            Nihihustle juu chini, ili nivuke boarder!
            Vinyaunyau hawa, wanasema niko out of order!
            Madharau haifai, japo naendesha bodaboda.
            Sinione leo hivi, kesho ngazi nitakweya.

Ni gani machoni mwako, huwa haikupendezi?
Ni nini puani mwako, vizuri hainukii?
Ni vipi domoni mwako, ladhake huwa shubiri?
Ni ipi kwa masikio, ja muziki haisikiki?
Kuna vyangu vigusavyo, ja kinyesi ukahisi?

            Toa maneno kutoa, shida yako tuijue
            Sema makosa ‘loona, alo nayo jikosowe
            Ukishindwa uandike, watakao wayasome.
            Amri sipoitii, litakurukia tope
            Wakakuita kasuku, maneno mengi matupu
            Au mbuni wakuite, aliaye pasi kitu.


One uria ararira aigua ni uramutiga
Aigua uramute tondu ari na thiina
Tiga kumute mwonereerie njira
Wahota kueheeria mundu ungi thiina
Ni aingi makoragwo na issues na ciake
Na life ciao ituraga na bugudha/iriro.

Ewe mwenzi nakusihi, una mawili sikiza
Kinyongo wala kijicho, kwako wewe mie sina
Sijakutakia mawi, ila yote yalo mema
Na popote duniyani, uwe mtu kutukuka
Labda leo telezi, kesho takuwa imara
Nenda kwa utaratibi, uendako ukufike
Sisi sote tafurahi, mwenzetu kafaidika.
                               
                        Okariithi@2012



2 comments:

  1. Great move keep it that way at least people can read this all over the world though they cannot read the vernacular the way its supposed to be may you can go a step further and recite on You Tube.

    ReplyDelete
  2. We think BEST in our first languages. Each translation loses a percentage of its authenticity. He who wishes to imbibe it better ought to learn a little of my/our roots. Otherwise,no regrets for being who we are for thats our 'uncontaminated' purity. Haujambo lakini bwana Kimathi? Usanii wako wa hali ya juu mbona umeusheheni pasipofikika siku hizi?

    ReplyDelete